Msanii mkongwe wa muziki wa Taarabu nchini Tanzania, Khadija Kopa maarufu kama Malkia wa mipasho amesema kuwa hana muda mrefu na yeye anaachana na muziki huo na kujikita zaidi kwenye mambo ya dini yake ya kiislamu.
Akiwa mbele ya Waandishi wa Habari, amesema kuwa hata akiacha muziki hata tangaza kama Mzee Yusuf alivyofanya bali ataacha kurekodi nyimbo na kupotea kimya kimya.
Kwa upande mwingine Bi. Kopa amesema kuwa muziki wa taarabu umeanza kupoteza ladha yake kama ilivyokuwa zamani hii ni kutokana wasanii wengi kubweteka na kuendekeza uvivu.
Mwaka 2017 gwiji wa muziki wa taarabu nchini Tanzania, Mzee Yusuf alitangaza kuachana na muziki huo na kumrudia Mwenyezi Mungu.
28 May 2018
New