Maafisa Wakuu wa NYS Nchini Kenya Wakamatwa kwa Ufisadi - MULO ENTERTAINER

Latest

28 May 2018

Maafisa Wakuu wa NYS Nchini Kenya Wakamatwa kwa Ufisadi

Maafisa Wakuu wa NYS Nchini Kenya Wakamatwa kwa Ufisadi
Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa nchini Kenya (NYS) Richard Ndubai, pamoja na maafisa wengine wakuu, wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za ufisadi.

Hii inafuatia agizo la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma aliyeagiza kushtakiwa kwa washukiwa wote waliotajwa katika kashfa ya Shilingi bilioni 9.

Maagizo ya Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma Noordin Haji yametolewa baada ya kupokea taarifa kuhusu kampuni 10 na pia zaidi ya watu 40 binafsi waliotajwa katika sakata hiyo NYS scandal kutoka kwa Mkurugenzi wa uchunguzi wa Uhalifu George Kinoti.

"Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka ya Umma amechunguza nyaraka zinazohusiana na sakata inayoendelea katika NYS na ameagiza mashtaka yafunguliwe mara moja dhidi ya wite waliotajwa kushukiwa ," iliandika ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumatatu asubuhi.

Washukiwa wengine kadhaa pia wamekamatwa na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani katika kipindi cha saa 24, kulingana na afisa mmoja katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

Pesa hizo zinadaiwa kuchukuliwa kutoka kwenye shirika hilo katika kipindi cha miaka mitatu, kwa mujibu wa duru mbali mbali.

Sakata hiyo inadaiwa kutekelezwa katika mpango uliowahusisha maafisa wa ngazi ya juu wa serikali na 'wauzaji hewa' na pigo jipya kwa juhudi za rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika juhudi zake za kukabiliana na ufisadi.