PICHA: Rais Magufuli Alivyokutana na Kufanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana - MULO ENTERTAINER

Latest

28 May 2018

PICHA: Rais Magufuli Alivyokutana na Kufanya Mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27 Mei, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli alipokea salamu kutoka kwa viongozi wa chama na Serikali wa Afrika Kusini na Zimbabwe ambako hivi karibuni Ndg. Kinana aliongoza ujumbe wa viongozi wa CCM kutembelea nchi hizo na kukutana na viongozi wakuu wa vyama tawala vya ANC na ZANU-PF vinavyoongoza Serikali.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli na Ndg. Kinana wamezungumzia maandalizi ya vikao vya Kamati Kuu ya CCM (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) vitakavyofanyika  tarehe 28-29, Mei, 2018 Jijini Dar es Salaam.