Serikali Yasema Gharama ya Kuunganisha Umeme ni 27000 Pekee - MULO ENTERTAINER

Latest

26 May 2018

Serikali Yasema Gharama ya Kuunganisha Umeme ni 27000 Pekee

SERIKALI  Kupitria kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu imesema gharama ya kuunganishia umeme ni Sh27, 000  tu.

Mgalu  amesema hayo jana bungeni Mei 25, 2018 wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge walizozitoa wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati ya mwaka 2018/19 .

Mgalu ameagiza makandarasi na wasimamizi wa miradi ya umeme vijijini (Rea) kuwashirikisha viongozi wa maeneo wanaposambaza umeme ili kuainisha maeneno yenye kipaumbele.

Alisema wamepokea ushauri wote uliotolewa ikiwamo suala la baadhi ya vijiji na maeneo yenye taasisi nyeti kurukwa kutokana na kutokuwapo ushirikishwaji.