SPIKA wa bunge, Job Ndugai ameitaka Wizara ya Fedha na Mipango kujitathmini kutokana na lawama ambazo imekuwa ikidaiwa kuchelewa fedha za bajeti, malipo, miradi na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali kwa wananchi wake.
Ndugai ameyasema hayo leo Bungeni kufuatia Mbunge wa Mtama Nape Nnauye kuomba Muongozo kuhusu Export Level ambayo inakatwa kwa wakulima korosho.
Awali wakati wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Nape aliomba jambo hilo lipelekwe kwenye Kamati ya Bajeti ili kuikutanisha Serikali, Wizara ya Kilimo na Wabunge wenye maslahi na hoja hiyo, lakini jambo hilo lilishindikana kuzungumzika kwenye kamati kutokana na kuwa nje ya kanuni za bunge ambapo leo Nape amelirudusha lijadiliwe Bungeni.
Hatua hiyo ya Nape imekuja kufuatia baada ya madai kuwa Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba ameilalamikia Wizara ya Fedha kwa kuchelewa kutoa fedha hizo za makato ya korosho za wakulima kwenda Wizara ya Kilimo, jambo ambalo limekuwa na ugumu kwa wizara yake kupewa fedha hizo.
“Hili ni moja ya mambo ambayo yanasikitisha sana, Waziri wa Kilimo alipoenda kwenye kikao cha Kamati ya Bajeti ilibidi atoe machozi, mtu analaumiwa wala siyo mkosaji, hawa watu ni hela zao. Kwa nini ukae na hela ya mtu? Akuombe, akupigie magoti, akulambe lambe? Wizara ya fedha mjitathini, mnawaumiza sana mawaziri sisi huku tunawaona hawafai kumbe nyie ndiyo vikwazo,” alisema Ndugai.
Hata hivyo, spika amesema anamsubiri waziri Mkuu kassim Majaliwa ili azungumze naye kuhusu suala hilo na endapo hawatal;iopatia ufumbuzi watalirejesha bungeni ili wabunge waamue.
24 May 2018
New