Wakali kutokea kwenye industry ya Bongo Fleva Vanessa Mdee pamoja na Barnaba wanategemea kuja kivingine katika mdundo mpya na hii ni baada ya picha zao kusambaa katika mitandao ya kijamii wakionekana wakiwa uswahilini wakiwa location.
Ukiachilia mbali ukaribu uliopo kati ya Vanessa Mdee pamoja na Barnaba nikufahamishe tu kuwa wawili hao walishawahi kukaa na kutoa ngoma kwa pamoja “Siri” mwaka 2015 na ngoma hiyo ilifanya vizuri ndani ya Afrika.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Vanessa Mdee pamoja na Barnaba kutoa ngoma ya pamoja na mashabiki wa wakali hawa wakae tayari kuipokea ngoma hii yenye maudhui ya uswazi ingawa wengi hawakutegemea kumuona Vanessa Mdee kushiriki kwenye nyimbo kama hizo kutokana na wengi kumuweka kwenye fungu la watu wenye maisha ya kizungu.
28 May 2018
New
mulo
Vanessa