Ashitakiwa Kwa Kujiita Mtoto wa CAG na Kisha Kubaka - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Ashitakiwa Kwa Kujiita Mtoto wa CAG na Kisha Kubaka

Ashitakiwa Kwa Kujiita Mtoto wa CAG na Kisha Kubaka
Mkazi wa Mwananyamala, Ahmed Mudhihiri (26), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni,   Dar es salaam akikabiliwa na mashtaka matatu yakiwamo ya ubakaji na kufanya udanganyifu kuwa yeye ni mtoto wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, Mwendesha Mashtaka, Neema Moshi, alidai Julai 6  katika eneo la Hoteli ya White Sands  Mbezi Africana   Dar es Salaam, mshitakiwa alimbaka binti (jina limehifadhiwa).

Shitaka la pili ni kuwa  kati ya Juni 17 na Julai 7 mwaka huu   Dar es Salaam, alidanganya kuwa yeye ni Mwamvita Makamba.

Katika shitaka la tatu, mshitakiwa alidaiwa kati ya Juni 18 na Julai 7 mwaka huu, Dar es Salaam, alijitambulisha kuwa yeye ni Edd mtoto wa   CAG.