Chadema Yajitoa Kushiriki Uchaguzi Katika Jimbo la Liwale na Kata 37 Utakaofanyika Oktoba - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Chadema Yajitoa Kushiriki Uchaguzi Katika Jimbo la Liwale na Kata 37 Utakaofanyika Oktoba


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema huo ni Uamuzi wa Kamati ndogo ya Kamati Kuu iliyokaa jana Septema 18 jijini Dar kutafakari mwenendo mzima wa uchaguzi

Amesema sababu mojawapo ni kukiukwa kwa Katiba katika chaguzi zilizopita za marudio ambapo kuna baadhi ya watu walinyimwa haki yao ya msingi ya kupiga kura

Sheria inasema katika zoezi moja la uchaguzi mkuu mpaka uchaguzi mwingine mkuu, wapiga kura wataandikishwa mara mbili lakini mara ya mwisho wapiga kura wameandikishwa nchini ilikuwa Agosti 2015

Hivyo basi, wale wote ambao wamefikisha miaka 18 kuanzia Novemba 2015 hawajapewa haki yao ya msingi ya kupiga kura katika maeneo yaliyokuwa na uchaguzi wa marudio

Aidha, amesema "Tume haitekelezi majukumu yake kwa mujibu wa Katiba kwa sababu Serikali ya CCM inahofia sana kuwa wapiga kura wengi ni vijana wanaounga mkono vyama vya mageuzi"