Kocha yanga ajiunga na Singida United - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Kocha yanga ajiunga na Singida United

 Kocha yanga ajiunga na Singida United
Imeelezwa kuwa aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amejiunga na timu ya Singida United kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Nsajigwa amejiunga na walima alizeti hao huku akiendelea kuwa Msaidizi ambapo sasa atakuwa chini ya Mkuu wake, Hemed Morocco.

Kocha huyo amefikiana mwafaka na viongozi wa Singida United tangu aachie ngazi ikiwa ni miezi kadhaa sasa akiwa hana timu.

Ikumbukwe Nsajigwa alieleza kujiondoa Yanga baada ya kuwa na minong'ono kuwa alikuwa akiihujumu timu na kusababisha kupata matokeo mabovu.

Mbali na kuinoa Yanga, Sanjigwa pia aliwahi kuichezea Yanga ambayo ni bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Bara mara 27.