Hizi Hapa Mechi za Ligi Kuu Zitakazotimua Vumbi Leo - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Hizi Hapa Mechi za Ligi Kuu Zitakazotimua Vumbi Leo

Hizi Hapa Mechi za Ligi Kuu Zitakazotimua Vumbi Leo
Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea tena leo kwenye viwanja tofauti kuwaka moto.

Jijini Dar es Salaam mabingwa wa kihistoria katika ligi, Yanga, watakuwa wanacheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga, mechi ikianza saa 1 jioni.

Kuelekea mechi hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya kipute hicho dhidi ya wagosi wa kaya.

Aidha, katika Uwanja wa Samora huko Iringa, Lipuli itakuwa inaikaribisha Alliance School ya mwanza ambapo mechi itaanza majira ya saa 8 mchana.

Pia kunako dimba la Mwadui Complex wenyeji ambao ni Mwadui FC watakuwa wanacheza dhidi ya JKT Tanzania kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mechi hizi zote zitaruka hewani kupitia Azam TV

Mechi zingine ni

Biashara United vs Azam FC
Mbeya City vs Ruvu Shooting na
Ndanda FC vs Mtibwa Sugar