Inasikitisha Hawa wa Nitarejea Anatia Huruma Hali yake Mbaya...Pombe Yamwaribu Ini - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Sept 2018

Inasikitisha Hawa wa Nitarejea Anatia Huruma Hali yake Mbaya...Pombe Yamwaribu Ini

Inasikitisha Hawa wa Ntarejea Anatilia Huruma Hali yake Mbaya
Mwanadada Hawa ambaye amepata umaarufu baada ya kushirikiana na Diamond kwenye wimbo wa ntarejea ambaye pia ilidaiwa kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na Diamond kwa sasa yupo kwenye hali mbaya kiafya baada ya kusumbuliwa na tatizo la Inni.

Hawa anapitia mateso makali sana kutokana na tatizo hilo kwakuwa kwa sasa hawezi kula vizuri wala kulala kutokana na tumbo kujaa maji na muonekano wake kwa sasa anaonekana kama mtu mwenye mimba ya miezi tisa.

Kwa sasa Hawa anaishi maisha ya tabu kutokana na hapati matibabu yoyote zaidi ya kuhudhuria kriniki kwaajili ya kutolewa maji.

"Nilienda hospitali ya muhimbili walinieleza ini langu ni kubwa ninahitajika kupandikizwa na muhimbili hawana huduma hiyo ya kupandikiza ini ila walisema itaanza mwaka huu lakini sijui ni lini kwa sasa hatima yangu ni kunyonywa  maji kila yanapojaa" alisema kwa uchungu Hawa wa ntalejea huku akilia

Familia Ya Hawa akiongozwa na mama yake mzazi wanapambana ili kuinusuru Afya Ya Hawa,
amewaomba Watanzania, Wasanii Wenzake Na Wote wanaoguswa na Taarifa hizi kuweza kusaidia kwa kutoa mchango ili ili kuweza kuokoa maisha ya Hawa Kutoa Ni Moyo Sio Utajiri, Namba Ya Mama  Hawa Ni +255 762 31 35 87