Irene Uwoya na Dogo Janja Ndio Basi Tena? - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Sept 2018

Irene Uwoya na Dogo Janja Ndio Basi Tena?

Irene Uwoya na Dogo Janja ndio basi tena?
Jumatatu hii katika pitapita zangu mitaa ya Posta jijini Dar es salaam, nilisikia vijana wawili wakizungumza kuhusu kuumwa kwa msanii wa hip hop, Dogo Janja huku mmoja kati ya hao akimlaumu rapa huyo kwanini ameingia kwenye mahusiano na mwanamke aliyemzidi umri.

Habari ambazo zinasambaa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba rapa huyo hayupo kwenye maelewano mazuri na mke wake Irene Uwoya.

Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo kutoka Arusha kuumwa siku za karibuni na kupelekea kulazwa lakini mke wake ambaye ni msanii wa filamu amekuwa alionekana kula bata katika viwanja mbalimbali.

Baada ya kugundua mume wake huyo anaumwa mrembo huyo alipost picha ya rapa huyo mtandaoni na kum-wish birthday, ujumbe ambao ulitafsiriwa na wadau wa mambo kwamba haukuwa na uzito wowote.

Jumanne hii baada ya taarifa kuendelea kuzagaa kwamba wawili hao wameachana, mrembo huyo ameandika ujumbe mpya.

“Whatever you hear about me please believe it…I no longer have time to explain myself…you can also add some if you wantπŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰,” aliandika Irene.

Bongo5 bado inalifuatilia jambo hili kwa ukaribu ili kukuletea taarifa ambayo imekamilika.