New
Mwanamke asiye na baiskeli nyumbani au asiyejua kuendesha baiskeli anaonekana kuwa hafai.
Nchini Rwanda ambako baiskeli ni kifaa muhimu katika maisha ya wanawake katika eneo la Bugesera kusini magharibi mwa Rwanda.
Wakati wa kufunga ndoa Bi harusi mtarajiwa anaweza kufurahia hata kuacha mambo mengine kama mkoba wake au viatu vyake vizuri lakini hatafurahi ikiwa katika furushi la zawadi anazopeleka kwa bwanake hakutakuwa na baiskeli.
Donata Mukabaruta akiendesha baiskeli iliyosheheni madumu 5 ya maji;hii ni sehemu ndogo tu ya shughuli nyingi za nyumbani anazofanya kila siku kwa kutumia baiskeli
''Baiskeli ndiyo maisha ya kila siku hapa. Inatusaidia katika shughuli za nyumbani, yaani baiskeli ni jibu kwa kila swali katika kazi za nyumbani kama vile kwenda sokoni, kuchota maji au kutafuta lishe ya mifugo''.
Mwanamke asiye na baiskeli nyumbani au asiyejua kuendesha baiskeli anaonekana kuwa hafai. Kwa kifupi, mwendo ambao ungefanyika kwa saa moja huwa inakuchukua nusu saa tu ukitumia baiskeli.''
Ni katika wilaya ya Bugesera kusini mashariki mwa Rwanda-eneo tambarare ,rahisi sana kwa matumizi ya baiskeli.
Lakini kubwa zaidi hapa ni kwamba kabla ya ndoa, bi harusi lazima aweke baiskeli kama zawadi ya kwanza miongoni mwa zawadi nyingi anazompelekea mumewe
''Mimi niliolewa mwaka 2008, baiskeli niliinunua franga elfu 80 ni kama dolla mia moja hivi.
Lakini hakuna hata kufikiria sana kuhusu zawadi nyingine. Kitu cha kwanza unachofikiria ni kununua baiskeli miongoni mwa zawadi nyingi unazopelekea mumeo.
Baiskeli ni kitu cha lazima. Huo ndio utamaduni wetu na tunaamini kwamba ukishaipata una uhakika kwamba harusi haiwezi kuvunjika."
Ni eneo lenye kasi kubwa ya maendeleo kukiwa na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa kimataifa wa ndege na miundo mbinu mingine ikiwemo barabara .
Wanasema huu sio mwisho wa umaarufu wa baiskeli katika eneo hili kwani masharti ya ujenzi wa barabara lazima yazingatie watumiaji wa baiskeli.
Kila msichana hapa lazima ajue kuendesha baiskeli