Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, Amkimbia Asia Msangi East Africa Radio - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Sept 2018

Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, Amkimbia Asia Msangi East Africa Radio

Leo mapema kwenye saa 8:00 asubuhi, East Africa Radio kupitia kipindi chao cha East Africa Breakfast, walialikwa mgombea ubunge jimbo la ukonga kupitia Ccm Mwita Waitara, na Asia Msangi ambae anagombea kupitia Chadema.

Asia Msangi ndiye aliyekua wa kwanza kuja studio, awali mahojiano ilibidi yaanze saa 7:00 asubuhi, lakini Mwita Waitara hakuja kwa wakati hivyo basi wakalazimika kusogeza mbele muda wa mahojiano hayo..

Baada ya kumsubiri muda mrefu, hatimaye Mwita waitara aliwasili studioni hapo kwenye saa mbili kasoro hivi. Lakini hata hivyo mara baada tu ya kumuona Asia Msangi Waitara alikakataa kata kata kufanya mahojiano hayo, huku akijitetea kwa kusema taaratibu za chama eti haziruhusu. Juhudi za watangazaji wa kipindi hicho Scolah Kisanga, Charles William na Shabani Modriki kumshawishi Mwita Waitara ziligonga Mwamba, baada ya Waitara kuondoka studioni hapo akiwa mwenye ghadhabu kubwa.

Hata hivyo mahojiano yalifanyika na Asia Msangi pekee ndie aliyehojiwa. Akizungumza katika kipindi hicho, Bi Msangi amewaomba wakazi wa Ukonga, wa muamini na wampe nafasi ya kuwatumikia kwani anauwezo na amekua akifanya kazi na wanajamiii ya Ukonga kwa muda sasa.