Mimi Bado Kijana Nina Hamu Ya Kuolewa Tena- Khadija Kopa - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Mimi Bado Kijana Nina Hamu Ya Kuolewa Tena- Khadija Kopa

Mimi Bado Kijana Nina Hamu Ya Kuolewa Tena- Khadija Kopa
Malkia wa Taarabu na mipango nchini Bibie Khadija Omary Kopa ameibuka na kudai ana mpango wa Kuolewa Tena kwani yeye bado ni kijana na anapenda kuwa ndani ya ndoa.

Khadija Kopa ambaye tayari amekwisha olewa kwa mara tatu miaka ya nyuma ameweka wazi kuwa ana nia ya Shari kabisa ya Kuolewa ndoa yake ya nne siku za mbeleni.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Khadija Kopa ameweka wazi kuwa ingawa yeye ni kiana na anataka kuolewa Tena lakini hana papara kwa sasa.

Mimi nimeshaolewa ndoa nne na mume wangu wa mwisho aliyekufa alikuwa wa nne kwaiyo endapo Mwenyezi Mungu akileta mwenye heri lazima nitaolewa Lakini pia kama sitapata wa kunioa tena basi naendelea na Maisha Yangu na kazi zangu.

Halafu isitoshe Kuolewa hakunaga umri utakuta kibibi cha miaka sitini kinaolewa itakuwa mimi ambaye najiona kijana wa jana halafu pia sitaki kuzini ikitokea nafasi ya kuolewa lazima”.