Wasanii wa Tanzania ni Wanafiki Kuwazidi Wanasiasa- Yeriko Nyerere - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Wasanii wa Tanzania ni Wanafiki Kuwazidi Wanasiasa- Yeriko Nyerere

Wasanii wa Tanzania ni Wanafiki Kuwazidi Wanasiasa- Yeriko Nyerere
Moja ya wanaharakati mashuhuri Tanzania Yerico Nyerere amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa tanzania ni wanafiki kwa sababu wamekuwa wakipiga sana kelele kuhusu vitu vya watu wengine lakini sio kuhusu maswala ya wasanii wao wenyewe.

Yerico ameyasema hayo ikiwa leo ni siku ya tatu tangu msanii Maua Sama  kuwekwa ndani na pia Soudy Brown kwa kosa la kucheza wimbo wa iokote na kuonekana akiwa anakanyaga noti ya shilingi elfu 10 kitu mabacho jeshi la polisi linasema kuwa ni swala la kudharirisha noti ya Tanzania.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Yerico anasema ” wasanii wa tz kunsdi la wanafiki , huenda kuwazidi hata wanasiasa, siku ya tatu sasa maua sama na Soudy Brown wako mahabusu kwa kosa la cybercrime kuchezesha  na kukanyaga pesa lakini wasanii nchini ako kimya kana kwamba hakuna kitu.ngoja twende sie wanasiasa tukawasaidie.