MSAFARA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, umevamiwa na kundi la Morani wakimpokea na kumraki wakati akiwasili wilayani Monduli mkoani Arusha kwa ajili ya kampeni za Chama Chake zinazoendelea katika jimbo hilo leo.
Chadema wanamnadi mgombea wao Yohana Masiaya ambaye anapigania kiti cha Ubunge kwa kupitia jimbo la Monduli ambalo awali lilikuwa likishikiliwa na Mbunge wa Chadema, Julius Kalanga kabla ya kujivua Ubunge na kukihama Chama hicho kisha kukimbilia Chama cha Mapinduzi (CCM).