Netanyahu Asikitishwa na Ndege ya Urusi Iliyoangushwa na Majeshi ya Syria - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Sept 2018

Netanyahu Asikitishwa na Ndege ya Urusi Iliyoangushwa na Majeshi ya Syria

Netanyahu asikitishwa na ndege ya Urusi iliyoangushwa na majeshi ya Syria
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea kusikitishwa kwake na na vifo vya raia wa Urusi waliokowemo ndani ya ndege iliyoangushwa kwa bahati mbaya na vikosi vya serikali ya Syria.

Netanyahu amemwambia Rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa Syria ilipaswa kulaumiwa kwa kuiangusha ndege hiyo.

Maafisa wa Urusi awali waliishutumu Israel kwa kuhusika na kitendo hicho ambacho ilidai wangekilipiza kauli ambayo ilipingwa vikali na Netanyahu ambaye alisema kamwe vikosi vyake havijihusishi na matukio kama hayo.

Putin ameelezea tukio hilo kuwa ni la bahati mbaya na vikosi vyake havitarudi nyuma katika kuiunga mkono serikali ya Rais Bashar al-Assad.