Jumla ya vijana 12 ambao waliokolewa pangoni nchini Thailand mwaka huu watakuwepo katika uwanja wa Old Trafford hii leo kuishuhudia Manchester United ikicheza na Everton.
Vijana hao ambao ni wa kutoka timu moja ya vijana nchini humo, waliokolewa kwa pamoja mwezi Julai baada ya kukwama kwa takribani wiki mbili katika pango lililojaa maji.
Tukio hilo liliteka hisia za watu wengi sehemu mbalimbali duniani na kupelekea hadi Makamu Mwenyekiti mtendaji wa klabu ya Manchester United, Ed Woodward kuwaalika kuhudhuria katika moja ya mchezo.
Taarifa zinaeleza kuwa vijana hao walikutana na kocha Jose Mourinho jana Jumamosi.
Kabla ya mchezo huo kuanza, vijana hao watapata nafasi ya kutembea pembezoni mwa uwanja huo wa Old Trafford.