Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, amepata ajali ya kuanguka stejini wakati akifanya shoo ya WASAFI FESTIVAL jioni ya leo Jumapili Desemba 09 katika Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga .
Kabla ya kupata ajali hiyo, Diamond alikuwa akiimba wimbo wa Zilipendwa akiwa na Mbosso na Rayvanny huku wakirukaruka ambapo ghafla ubao wa steji ulifyatuka na kusababisha Diamond na Rayvanny kuanguka chini ya steji, huku tukio zima likioneshwa moja kwa moja na Wasafi TV.
Hata hivyo hakuna madhara makubwa yaliyoripotiwa kwa upande wa Diamond na msanii mwenzake. Wasafi Festival ililazimika kurudiwa leo bure baada ya kujana kunyesha mvua kubwa iliyosababisha baadhi ya wasanii kushindwa kufanya shoo