Aliyeshika namba 1 matokeo form 4 aeleza machungu - MULO ENTERTAINER

Latest

25 Jan 2019

Aliyeshika namba 1 matokeo form 4 aeleza machungu

Aliyeshika namba 1 matokeo form 4 aeleza machungu
Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018, Hope Mwaibanje, ameelezeaa siri ya kufanya vyema, licha ya changamoto nyingi alizozipitia katika safari hiyo.

Akisimulia namna alivyokuwa akipambana ili aweze kufikia malengo yake ya kufaulu, Mwaibanje amesema  alilazimika kutumia kibatari kujisomea kutokana na nyumba wanayoishi kutokuwa na umeme.

Mwaibanje amesema, “makazi yetu ni ya kawaida kama unavyoyaona, tunaishi nyumba haina umeme na mimi nilipokuwa nikija likizo nilikuwa natumia kibatari kujisomea, niliona ni hali ya kawaida kwangu na nashukuru Mungu nimefanya vizuri katika matokeo yangu”.

“Shuleni kulikuwa na ushindani mkubwa katika masomo na mimi nilitokea shule za mtaani, ila nilijituma kutimiza nia yangu ya kuwa daktari bingwa wa moyo. Nikianza kidato cha tano nitasoma Fizikia, Kemia na Baiolojia,” ameongeza mwanafunzi huyo.