Jaji Mkuu asifu kesi ya Zitto kukataliwa - MULO ENTERTAINER

Latest

25 Jan 2019

Jaji Mkuu asifu kesi ya Zitto kukataliwa

Jaji Mkuu asifu kesi ya Zitto kukataliwa
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, amemsifu Msajili aliyesimama kidete kukataa kusajili ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe iliyokuwa inadaiwa kuwa na dosari.


Ametoa sifa hizo leo wakati akizungumzia kuhusu wiki ya Sheria mbele ya wanahabari.

"Namsifu Msajili aliyesimama kidete kukataa kusajili kesi yenye dosari, nampongeza kwa ujasiri, tuna Majaji wachache hatutaki kuwapangia kesi nyingi kisha wazifute" - Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim.

Hata hivyo, muwakilishi kutoka mahakama kuu, akijibu swali la kwa nini Msajili alikataa kusajili kesi ya Mbunge huyo, amesema, "Msajili hatarusu 'Human error' anapaswa kuangalia nyaraka zinakidhi vigezo vyote vya kimahakama. Kukiwa na makosa kutasababisha kesi kuchukua muda mrefu sana. Ni jambo la kawaida msajili kufanya "Screening" kabla ya kusajili kesi.

Ameongeza, "Kuna makosa ya kibinaadamu, lazima marekebisho yafanyike. Kesi ile ya juzi haikuwa ya kwanza wala ya pili".

Mbali na hayo, Jaji Mkuu ameeleza kuwa wanasiasa hawawezi kuzuiwa wasizungumze kwa kuwa hiyo ndiyo kazi yao.

Akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu maneno yanayosemwa na wanasiasa kwamba mahakama zimekuwa haziko huru na zimewekwa mifukoni, Jaji Mkuu amesema kwamba mahakama haiwezi kujibu suala hilo kwa kuwa wao wanafanya kazi kimyakimya.

"Sisi tunafanya kazi kimyakimya na ukitaka majibu utayakuta katika nyaraka”  Profesa Ibrahim