Straika wa timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta atatua katika Klabu ya MidÂdlesbrough ya England endapo klabu hiyo ikitoa kiasi cha Euro milioni 6.5 (bilioni 17) ambayo ndiyo thamani ya mchezaji huyo.
Samatta anayeongoza chati ya wafunÂgaji katika Ligi Kuu ya Ubelgiji akiwa na mabao 15, anawindwa kwa ukaribu na baadhi ya timu za EngÂland samÂbamba na Fenerbahce ya Uturuki.
Kwa mujibu wa takwimu za Mtandao wa viwango wa Transfermarket, unaonyesha kwamba thaÂmani ya nahodha huyo wa Taifa Stars imepanda maradufu kutoka ile aliyokuwa nayo Septemba, mwaka jana.
Kwa sasa Samatta anayeshika nafasi ya tano kwa ubora ndani ya kikosi cha Genk, amepanda thamani kutoka Euro milioni nne (sawa na bilioni 10), mwaka jana hadi bilioni 17 kwa mwezi huu.
Timu ambazo zinamtaka mshambuliaji huyo anayekamaÂta nafasi ya 183 duniani kwa wachezaji wanaocheza nafasi ya mshambuliaji wa kati, zitalazimika kuilipa KRC Genk dau hilo la bilioni 17, kwa ajili ya kuipata huduma yake.
Wakati Samatta ambaye ndani ya Ligi kuu ya Ubelgiji akikamata nafasi ya 14 kwa ubÂora wa viwango vya wachezaji thamani yake ikipanda, swahiba wake Thomas UlÂimwengu aliyejiunÂga na JS Saoura ya Algeria, mamÂbo hayÂaendi sawa baada ya thamani yake kushuka kutoka dola 150,000 hadi dola 100,000