Jeshi la Polisi Latoa Onyo Kwa Askari Wanaokiuka Maadili - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Jan 2019

Jeshi la Polisi Latoa Onyo Kwa Askari Wanaokiuka Maadili


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm, limewaonya Askari wake wachache wanaokiuka maadili ya Jeshi hilo kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, uonevu pamoja na kuwabambikia kesi wananchi kuwa hawatovumiliwa na hatua kali zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dsm Lazaro Mambosasa ametoa onyo hilo wakati akiwapongeza Askari 7 kati ya 38 waliofanya kazi kwa weledi na Ufanisi na kupandishwa vyeo na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Siro.

Aidha amewashukuru wananchi wa Dsm pamoja na wadau mbalimbali wanaoendelea kutoa ushirikiano katika suala la Ulinzi na Usalama, utoaji wa taarifa ya wahalifu na uhalifu hali ambayo imewezesha Jiji la Dsm kuendelea kuwa shwari.