Baada ya taarifa katika mitandao ya kijamii kuenea kwamba penzi la Diamond na mrembo wa Kenya, Tanasha lipo juu ya mawe. Mrembo huyo ambaye alitoa ahadi ya kuliweka penzi lake hilo private wiki hii ameibuka upya.
Wiki hii katika mitandao ya kijamii zilizagaa taarifa kwamba Diamond na Tanasha wameachana baada ya muimbaji huyo kutamka katika moja ya interview zake kwamba hata funga ndoa tena mwezi ujao.
Jana Tanasha ambaye ni mtangazaji wa la NRG alipost picha ya Diamond Instagram na kuandika ujumbe wa upendo.
Baada ya post hiyo Diamond alimjibu mrembo huyo kwa kuandika ujumbe kwa amemkumbuka sana.
Katika hatua nyingine Natasha alitumia Insta Story kukanusha uvumi wa kwamba ameachana na Diamond baada ya kuona Rais huyo wa WCB anampotezea muda.