Achiraf Hakimi Mchezaji nyota wa PSG afunguka mazito juu ya mpenzi wake kutaka kumfirisi. - MULO ENTERTAINER

Latest

3 Sept 2024

Achiraf Hakimi Mchezaji nyota wa PSG afunguka mazito juu ya mpenzi wake kutaka kumfirisi.

 Achrafu Hakimi Afunguka Alivyotaka Kufilisiwa na Mkewe Mahakamani


Imepita miezi kadhaa tangu siku ambayo mchezaji wa PSG ya Ufaransa, Achrafu Hakimi alipoamua kuachana na mkewe, Hiba Abouk huku taarifa za mali zake kuandikwa kwa jina la mama yake zikiwa zimesikika sana kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani.


Kuna mengi yalitokea ambayo yaliwafanya kuachana. Tangu kipindi hicho Hakimi hakuwa amezungumza chochote kilekilichojiri mpaka wiki hii alipoamua kuweka kila kitu wazi. Anasema:


“Nilikutana na mke wangu akiwa mtu wa kawaida kabisa, aliingia kwenye maisha yangu akiwa hana kitu chochote kile. Ndani ya miezi miwili ya ndoa nilianza kugundua kwamba mwanamke huyo alichokuwa amekifuata kwenye maisha yangu ni pesa.


“Ni kama kengele iligonga kichwani mwangu, nikaamua kuandaa mazingira ili kama kuna jambo litatokea basi mali zangu ziwe salama kabisa.


“Kuna siku tuligombana na akaniambia siku akiamua kudai talaka basi ataniacha nikiwa sina kitu kwa kuwa tutagawana mali. Maneno yake hayo yakaniingia kichwani na hapo ndipo nikaamua kuandishikisha mali zangu kwa jina la mama yangu.


“Nilimwambia mama kila kitu, yeye mwenyewe alihuzunika kwani hakutegemea na hiyo ndiyo sababu ambato ilimfanya kukubaliana nami mali zangu ziandike kwa jina lake.


“Siku alipoamua kuachana nami, mahakama ikafuatilia na kugundua mali zangu zote zina jina la mama yangu, hivyo hakutakiwa kuchukua chochote kutoka kwangu. Akawa analia mahakamani, hakulia kwa sababu ya kulia, aliliakwa sababu ya kukosa mali ambazo alihisi angezipata kutoka kwangu.


“Mpaka leo hii, sina hamu na mwanamke yeyote yule. Marafiki, wote watapita lakini upendo wa mama utaendelea kuwa vilevile mpaka anaingia kaburini.”