Diamond Platnumz sasa ni ‘hotcake’ kiasi cha kuwafanya wasanii wengi wa Afrika kutamani kufanya naye collabo, lakini kwa uamuzi mpya alioupitisha wasanii wa Nigeria ambao hawajafanikiwa kufanya nae wataikosa nafasi hiyo.
Platnumz ambaye Jumamosi iliyopita pamoja na msanii wa Afrika Kusini, Donald wameshoot video ya collabo yao mpya, amesema kwa sasa amefunga milango ya kupokea collabo za wasanii wa Nigeria. Hii inamaanisha zile collabo za wasanii wanaomuomba yeye afanye nao.
Diamond ameongeza kuwa collabo ya mwisho kutoka Nigeria ni ile ya Kcee na yeye iliyotoka hivi karibuni, ambayo wanatarajia kuifanyia video nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo Diamond amesema miongoni mwa wasanii wengine wa Afrika ambao wametuma maombi ya kufanya naye collabo ni pamoja na Ferré Gola pamoja na kundi la Too Fan la Togo.

- “Sababu ya kusimamisha kwa sasa isiwe too much too much “ amesema Diamond kupitia 255 ya Clouds Fm. “ kwasababu mwanzo tulikuwa tunafanya collabo na watu kwasababu ya kutafuta tobo la kuingia Nigeria, tumeishaingia vizuri Nigeria tunakubalika tunafahamika na nyimbo zetu zinafanya vizuri hata tukitoa nyimbo ambazo tunatoa wenyewe tu zinahit, mfano kama Nasema Nawe navyokwambia sasa hivi inafanya vizuri Nigeria, so inakuwa haina maana kila mtu akushirikishe shirikishe unakuwa hauna umuhimu, zimebaki tu baadhi ya collabo za ambazo za wasanii wanaofanya vizuri zitatoka baadae lakini sio kwasasa hivi kwani tumezisimamisha, kwani tumekuwa tukiombwa sana sana sana na wasanii wa Kinigeria kufanya collabo tumesimamisha.”
Diamond ameongeza kuwa collabo ya mwisho kutoka Nigeria ni ile ya Kcee na yeye iliyotoka hivi karibuni, ambayo wanatarajia kuifanyia video nchini Afrika Kusini.
- “katika nyimbo ambazo tumeshirikishwa itakuwa ya mwisho hii tumefanya na Kcee kwa sasa ambayo kuanzia kesho tunaanza kushoot video yake ambayo inafanyika hapa hapa South Africa, ilitakiwa tushoot Mozambique lakini kwasababu nina issue za kifamilia hapa South Africa imeshindikana kwenda Mozambique imebidi nimwambie inabidi tushoot hapa hapa.”
Hata hivyo Diamond amesema miongoni mwa wasanii wengine wa Afrika ambao wametuma maombi ya kufanya naye collabo ni pamoja na Ferré Gola pamoja na kundi la Too Fan la Togo.