TETESI:Lowassa Aandaa Waraka Kumchanachana Kikwete, Kisha Kutimkia Ng'ambo... - MULO ENTERTAINER

Latest

21 Jul 2015

TETESI:Lowassa Aandaa Waraka Kumchanachana Kikwete, Kisha Kutimkia Ng'ambo...

Hatimaye mbunge wa Monduli Edward Lowassa kesho atatoa waraka mzito utakaoelezea namna ambavyo alifanyiwa kile alichokiita 'hila' na rais Kikwete.

Waraka huo unatarajiwa kulitikisa taifa na huenda ukaigawa vibaya CCM.

Baada ya waraka huo pia Edward Lowassa anatarajiwa kutoa rasmi hatima yake kisiasa huku kila dalili ikionyesha kuwa ataisambaratisha vibaya CCM kutokana na maamuzi atakayochukua.

=======
UPDATES:

- Miongoni mwa mambo mazito yaliyo kwenye waraka huo ni hatua ya Edward Lowassa kumuunga mkono Dr. Willbrod Slaa kama mgombea urais anayekubalika na wengi baada ya yyeye kuenguliwa.

- Pia kuna dalili (ingawa siyo za wazi na zimetawaliwa na giza nene kwamba huenda Lowassa atatangaza rasmi kuhamia Chadema ingawa hatagombea urais).

- Taarifa nyingine zinabainisha kuwa EL baada ya kubwaga manyanga, atatimkia ng'ambo wakati CHADEMA wakimwandalia mapokezi "mazito"