Christian Bella aka ‘King of Best Melodies’ amesema bado yupo njia panda kuchukua uraia wa Tanzania huku akiimarisha zaidi makazi ya nyumbani kwao.
Bella anayetamba kwa sasa na video ya Nashindwa, ameiambia Bongo5 leo kuwa ingawa amekuwa akipokea ushauri kutoka kwa watu wa karibu lakini bado anaona kwa sasa sio muda sahihi.
“Kupata uraia sio kitu rahisi,” amesema. “Naichukulia Tanzania kama nyumbani kwangu, tena najisikia furaha zaidi kwa sababu ni sehemu ambayo imenipa nafasi ya kufanya kile ninachokipenda maishani mwangu. Umaarufu nilionao Tanzania sio umaarufu nilionao Kongo. Wengi wamekuwa wakinishauri nichukue uraia lakini naogopa nisije nikajuta baadaye. Acha niendelee kutafakari kwanza, ikifika wakati basi hakuna kinachoshindikana,” ameongeza.
Pia Bella amesema kitu kingine kinachomuumzia ni kukaa mbali na mke wake pamoja na mtoto wake wanaoishi nchini Sweden.
“Hii inanicost sana ninavyotaka kuonana nao. Sipendi niache familia yangu huko Ulaya na mimi nipo Bongo, yaani mtoto na mama yake wananimiss sana na mimi nawamiss sana. Lakini kikwazo ni mtoto anasoma na serikali ya kule inafuatilia sana watoto, huwezi kumtoa mtoto wako akae nje ya shule kwa miezi mitatu. Mtoto wanachukulia kama wa kwao hivi na mimi najua sio kitu kizuri kuacha familia yangu mbali na mimi nipo huku lakini ndo maisha,” amesema.
“Mimi muziki wangu unapendwa huku na sio kule. Hata nikienda kule na rangi hii nyeusi wataleta dharau,.”