Wanawake Mnavuruga Ndoa Sababu ya Kujilinganisha na Wanaume - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Aug 2015

Wanawake Mnavuruga Ndoa Sababu ya Kujilinganisha na Wanaume

Zamani enzi za wazazi wetu wanawake walikuwa wakiona kuwa mwanaume ni kichwa cha familia na kiongozi na walikuwa wakiheshimu waume wao sana kwakuwa waliwasikiliza waume wao.

Hili lilipelekea wazee wetu kudumu katika ndoa kwakuwa hawakutaka usawa yani kujilinganisha na wanaume.

Kizazi cha sasa baadhi ya wanawake wengi wamekuwa wakitaka usawa wa kuongoza familia yani kujilinganisha na wanaume hawawasikili wanataka wao wasikilizwe tu.

Mfano kuongoza familia, utakuta mwanamke anampelekesha mumewe kwa kila kazi za nyumbani yeye kajikalisha.

Utakuta maelewano ndani ya ndoa hamna kwakuwa yale anayotakiwa kufanya baba mama nae anataka afanye.

Mwananamke usitake kujilinganisha na mwanaume kwa chochote kumbuka Biblia inasema ulitoka kwenye ubavu wa mwanaume.

Nawasihi wanawake heshimuni waume zenu acheni kujilinganisha na wao, mnapaswa kujua kuwa mwanaume ni kichwa cha familia ni kiongozi hivyo aheshimiwe.

NB: Mwanamke mpumbavu ataivunja ndoa kwa mikono yake mwenyewe. Pia tujifunze kumtumia MUNGU awe kiongozi wa ndoa zetu.

MUNGU awabariki,Jumapili njema