Mbwana Samatta Ateuliwa Kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika, ni Wachezaji Wanaocheza Soka la Ndani - MULO ENTERTAINER

Latest

12 Oct 2015

Mbwana Samatta Ateuliwa Kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika, ni Wachezaji Wanaocheza Soka la Ndani

Mshambuliaji wa Taifa Stars na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samatta ameteuliwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika inayowahusu wachezaji wanaochezea vilabu vya ndani ya Afrika.

Orodha hiyo imetolewa jana Jumapili na shirikisho la soka barani Afrika, CAF.

Samatta aliiwezesha TP Mazembe hivi karibuni kuingia kwenye fainali ya michuano ya mabingwa wa Afrika. Mazembe itakutana na USM Alger ya Algeria kwenye fainali.

Kupitia Instagram, Samatta ameandika: List ya wanaowania mchezaji bora wa mwaka wa Africa kwa wanaocheza ndani ya Africa nashukuru mungu nimekuwa nominated katika hao# dua zenu ili ikiwezekana iangukie TANZANIA#vb#.”

Samatta ni miongoni mwa wachezaji wa Taifa Stars walioivaa Malawi jana na kusonga mbele kwenye hatua za awali za michuano ya kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Full list:

1.Abdeladim Khadrouf (Moghreb Tetouan, Morocco) Morocco

2. Abdelmalek Ziaya (ES SETIF, Algeria) Algeria

3. Ahmed AKAICHI (Espérance de Tunis, Tunisa) Tunisia

4. Andiramahitsinoro Carolus (USMA, Algeria) Madagascar

5. Baghdâd Bounedjah (Etoile du Sahel, Tunisia) Algeria

6. Bakri el Madina (El Merriekh, Sudan) Sudan

7. Bassem Morsi (Zamalek, Egypt) Egypt

8. Boris Moubhio (AC. Leopards, Congo) Congo

9. Djigui Diarra (Stade Malien, Mali) Mali

10. Felipe Ovono (Orlando Pirates, South Africa) Equatorial Guinea

11.Guelassiognon Sylvain GBOHOUO (T.P Mazembe, D.R Congo) Côte d’Ivoire

12.Hazem Emam (Zamalek, Egypt) Egypt

13.Hocine Ragued (Espérance de Tunis, Tunisia) Tunisia

14.Kermit Erasmus (Orlando Pirates, South Africa) South Africa

15.Malick Evouna (Al Ahly, Egypt) Gabon

16.Mbwana Aly Samatta (T.P Mazembé, D.R Congo) Tanzania

17.Mohamed Koffi (Zamalek, Egypt) Burkina Faso

18.Mohamed Meftah (USMA, Algeria) Algeria

19.Moudather el Tahir (AL HILAL, Sudan) Sudan

20.Oupa Manyisa (Orlando Pirates, South Africa) South Africa

21.Robert Kidiaba (T.P Mazembe, D.R Congo) D.R Congo

22.Roger Assalé (T.P Mazembe, D.R Congo) Cote d’Ivoire

23.Thamsanqa Gabuza (Orlando Pirates, South Africa) South Africa

24. Zein Edin Farahat (USMA, Algeria) Algeria