Wastara |
Kwa mujibu wa chanzo makini, Marry ambaye anadaiwa kuishi Dubai, baada ya kuona lengo lake halijatimia, alianza kutoa maneno ya kashfa kwa Wastara kupitia mitandao ya kijamii, akidai ameingia mitini baada ya kuchukua pesa kutoka kwake.
“Huyo Marry ambaye alikuwa rafiki wa Wastara anadai alimtumia pesa ili amnunulie dawa za mwanaye, lakini hakufanya hivyo na badala yake, akawa hapokei simu akipigiwa na vilevile ‘akamblock’ kwenye mtandao wa WhatsApp, ndipo huyo dada akakasirika na kuamua kuropoka,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta Wastara na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, ambapo alikiri kutokea, kwani Marry aliyefahamiana naye kabla hajaondoka nchini, alimtumia fedha shilingi laki tano kwa ajili ya kununua dawa za mwanaye, lakini alipomtaka amuelekeze kwa ndugu zake wanaoishi Kenya ili azipeleke, alikataa.
“Wakati nilipokwenda Kenya kwenye matibabu ya mguu wangu, alinitumia tena shilingi laki mbili kunisaidia, lakini siku chache baadaye nikaanza kushangaa ananipigia simu na kunitumia picha akiwa mtupu, akinishawishi tufanye mapenzi ya jinsia moja, kitu ambacho kiliniudhi na kuamua kuacha kupokea simu zake na pia nikamzuia katika akaunti yangu ya WhatsApp,” alisema Wastara.
Kwa upande wake, Marry kupitia mawasiliano kwa njia ya mtandao huo, alionesha kushangazwa kwake na mabadiliko ya tabia ya Wastara, kitu ambacho hata hivyo hakimshtui isipokuwa anahitaji kurejeshewa fedha zake.
“Sasa sielewi kwa nini tangu nimtumie zile pesa hataki kuongea na mimi, hayo mambo ya usagaji hata sielewi maana mimi ni mwanamke, nina jinsia moja, sina jinsia ya kiume, nitafanyaje mapenzi na yeye, nachotaka anipe pesa zangu, simuogopi hata kidogo,” alisema.