Magesa Mulongo: Dr. Faisal ni 'Msomali' anayeishi Tanzania kwa uraia wa kutatanisha - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Jan 2016

Magesa Mulongo: Dr. Faisal ni 'Msomali' anayeishi Tanzania kwa uraia wa kutatanisha

                              

Hatimaye chanzo cha ugomvi kati ya mkuu wa mkoa wa Mwanza ndugu Magesa Mulongo pamoja na aliyekuwa msaidizi wake mkuu kwenye masuala ya kiutawala Dr. Faisal ambao ulipelekea Dr. Faisal kufukuzwa kazi na rais Magufuli kimebainika.

Ilielezwa awali kuwa kulikuwa na ugomvi ambao kulipelekea Dr. huyo kufukuzwa kazi kati yake na mkuu huyo wa mkoa. Vyanzo vyangu vimefanikiwa kudodosa kwa Mulongo kuwa Dr. Faisal ni nani hasa ambapo Mulongo amefunguka bayana kuwa Dr. Faisal ni raia kutoka Somalia anayeishi Tanzania kwa uraia unaotia shaka!

Ndugu Mulongo anakiri kuwa walitofautiana ndani ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha mkoa ndipo akaamua kumporomoshea Dr. huyo lugha za ubaguzi kuhusu uraia wake. Aidha uchunguzi wa kina unabaini kuwa viongozi hao wawili walikuwa na ugomvi wa muda mrefu kiutendaji kutokana na ndugu Mulongo kumtuhumu Dr. Faisal kuwa ni mfuasi wa Edward Lowassa na alifanya naye kikao cha pamoja mwezi wa sita mwaka jana!

Maneno ya kibaguzi kwa ndugu Mulongo yanakuja siku chache sana baada ya ujumbe wa kibaguzi kutolewa kutoka kwa wana UVCCM Zanzibar waliotoa ujumbe "CHOTARA HIZBU, ZANZIBAR NI YA WAAFRIKA" ambapo ujumbe huo ulitafsiriwa kama ubaguzi kwa Wapemba wenye asili ya kiarabu waishio visiwani humo.