Ofisi ya Kamishna Mkuu TRA Yavunjwa, Kompyuta Mbili Zaibiwa - MULO ENTERTAINER

Latest

20 Jan 2016

Ofisi ya Kamishna Mkuu TRA Yavunjwa, Kompyuta Mbili Zaibiwa

Watu wasiojulikana  wamevamia  na  kuvunja  ofisi  ya  kamishna Mkuu wa Mamlaka  ya  Mapato  Tanzania (TRA) na kuiba kompyuta  na  vifaa vingine.

Habari tulizozipata ambazo zimethibitishwa  na Polisi kanda maalumu  ya  Dar  es  Salaam zinasema miongoni mwa kompyuta zilizoibiwa  ni  ile  iliyokuwa  inatumiwa  na  Dr Philip Mpango  alipokaimu nafasi ya  Kamishna mkuu wa TRA  kabla ya kuteuliwa  kuwa  Waziri  wa  Fedha

Kwa mujibu wa chanzo hicho,huenda kompyuta hiyo ikawa na taarifa muhimu kuhusu ukwepaji wa kodi  na  sakata  la  makontena  Bandarini.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu  Ya Dar es salaam,Simon Sirro amesema tayari jeshi hilo  linawashikilia  watu  wanne  kwa  uchunguzi  zaidi

Siro  alitaja  vitu  vilivyoibwa  katika  ofisi  hiyo  kuwa  ni  Kompyuta  mbili, Televisheni  moja  na  King'amuzi.

Alisema  wanaoshikiliwa  ni  walinzi  wawili  kutoka  kampuni  ya  Suma JKT ambao  walikuwa  zamu  usiku huo, Katibu Muhtasi  pamoja  na  Karani  wa  Ofisi  hiyo.