Katika hali isiyo ya kawaida nimegundua kuwa mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu na kuweza ku-access mawasiliano yangu yote hasa ya sms tokea mwezi wa 10 mwaka jana 2015 na kuzihifadhi kwenye simu yake.
Sina uhakika kama aliweza kupata mawasiliano mengine tofauti na sms.
Ninasema ku-hack kwa sababu tunaishi mikoa tofauti na hivyo hakuwa na namna yoyote ya ku-access simu yangu physically toka wakati huo, pia simu yangu ambayo ni smart phone ina security (password) in case angetumia mtu aliye karibu yangu.
Nimegundua hii hacking baada ya kuwa na hali ya kutoelewana kati yetu kwa muda sasa ambapo pamoja na mambo mengine niligundua kuna taarifa zangu za siri anazozifahamu ndipo nilipoanza uchunguzi na kugundua kuwa ana hizo sms.
Miongoni mwa sms anazoshikia bango ni zile zinazohusiana na miamala ya Mpesa ambapo nimewatumia pesa ndg, jamaa na marafiki ambao sikuona umuhimu wa kumtaaifu hivyo akazijengea hoja mbali mbali ikiwemo ya uhusiano wa kimapenzi wakati si kweli!
Nimejaribu kumbana aseme amewezaje ku-access "private communications" zangu ila amegoma kabisa kuweka wazi.
Cha kushangaza zaidi ni kuwa hana utaalam wowote wa masuala ya mawasiliano!
Kwa kuzingatia usumbufu uliojitokeza kwa kuingilia mawasiliano yangu ya siri hasa kupitia mis-perception ya taarifa alizokutana nazo, nimepata wazo la kumshtaki kwa mujibu wa ile SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015 ila nikaona kabla sijafanya hivyo nililete suala hili hapa ili nipate michango yenu ya mawazo hasa juu ya nini cha kufanya.
Suala hili limenichanganya sana hasa ukizingatia kuwa tumekuwa kwenye ndoa takribani miaka 8 sasa na tuna watoto 2.
Naombeni michango yenu ya mawazo.
Ahsante!