Picha ya Tukio jingine |
Akielezea mazingira ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilfred Mutafungwa amedai kuwa Akyo alichapwa viboko 70 na wazee hao wa kimila wa Kimeru na Kimasai.
Mutafungwa amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwezi uliopita wakazi wa Kata ya Karansi wilayani hapa walitoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.