Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya Afariki Dunia Kwa Ajali ya Gari leo - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Oct 2016

Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya Afariki Dunia Kwa Ajali ya Gari leo

Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya, Maendekleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hellen Semi amefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea leo Chalinze mkoani Pwani.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, msemaji wa Wizara ya Afya, Maendekleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Nsachris Mwamwaja amesema amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi ambapo maofisa hao walikuwa wakielekea Dodoma kuhudhuria mkutano wa Waganga wa Mikoa unaotarajiwa kuanza kesho.


Mbali na Mkurugenzi huyo aliyefariki, Dk Neema Rusibamayila ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya alijeruhiwa katika ajali hiyo.