Q-CHIEF Adai Patoranking Kasababisha Mpango Wake wa Kuoa Hivi Karibuni Usogee Mbele - MULO ENTERTAINER

Latest

15 Nov 2016

Q-CHIEF Adai Patoranking Kasababisha Mpango Wake wa Kuoa Hivi Karibuni Usogee Mbele

Msanii mkongwe katika tasnia ya bongo fleva Q Chief amefunguka na kusema kuwa haikuwa jambo dogo na jepesi kufanya collabo na msanii Patoranking kutoka nchini Nigeria.

#Chillah amedai kuwa pesa nyingi zimetumika kufanikisha collabo hiyo kiasi cha kufanya hata mpango wake wa kuoa usogee mbele.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio Q Chief anadai kuwa pesa za kutosha zilitumika jambo ambalo limefanya ashindwe kutimiza ahadi yake aliyowahi kuitoa kuwa ataoa siku za karibuni.
.
“Kiukweli namshukuru sana Qs Mhonda kwani alisimamia hili, kiukweli pesa ya kutosha imetumika kukamilisha kazi hii, hivyo haikuwa rahisi mimi kufanya na #Patoranking maana wenzetu wanaangalia wapi wametoka na wapi wanataka kwenda, wanafanya kazi na nani kwa maslahi gani, hivyo kabla ya kufanya kazi na wewe wanafanya utafiti wa kutosha, hata yeye alijaribu kunitafuta kwenye mitandao, na kuona kazi zangu akaona nafanya nini, aliangalia kama niko marketable baada ya hapo aliporidhika tukafanya kazi” alisema QChief