Rose Ndauka Atetea Kuvunjika Kwa Ndoa Yake...Adai ni Tatizo la Jamiii - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Nov 2016

Rose Ndauka Atetea Kuvunjika Kwa Ndoa Yake...Adai ni Tatizo la Jamiii

Malkia wa filamu Rose Ndauka amewataka watanzania kujua kuvunjika kwa ndoa sio tatizo la wasanii wa filamu pekee bali ni tatizo la jamii nzima.

Mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae, Naveen amesema kwa sasa yeye bado yupo yupo kuingia kwenye maisha ya ndoa.

“Ndoa ni makubaliano ya watu wawili, mimi bado nipo nipo kidogo,” Rose alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM “Tusiwatazame tu bongo movie hata kwenye jamii ya watu wa kawaida ndoa hazidumu zinavunjika,”

Mwigizaji huyo mwaka uliopita aliachana na mpenzi wake aliyezaa naye mtoto mmoja mwenzi mmoja kabla ya tarehe waliotangaza kufunga ndoa.