Tuhuma za Chama Tawala na Serikali kuhonga wabunge - MULO ENTERTAINER

Latest

3 Nov 2016

Tuhuma za Chama Tawala na Serikali kuhonga wabunge


Hongera sana Freeman Mbowe kwa kukitumia Vyema Kiti chako kama Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuanika Unafiki wa Serikali na Chama Tawala.
Kitendo cha Kumuuliza Waziri Mkuu juu ya Ukweli wa Tuhuma za Chama Tawala na Serikali kuhonga wabunge wa Chama Tawala Milioni 10 ili wapitishe Mswada wa ovyo na Kandamizi wa Huduma ya Habari,badala ya Naibu Spika Kuruhusu Waziri Mkuu kujibu Tuhuma akatumia kiti chake Kuilinda serikali na kuendelea kuboresha mazingira ya Ufisadi na Ukiukwaji mkubwa wa Maadili Bila Aibu.
Wanaharakati,Wanahabari na Watanzania kwa Ujumla tuungane kupaaza sauti nje ya Bunge kukataa Bunge letu kutumika kama zulia la Mlangoni kufutia tope la Ufisadi(Doormart).
Katika Wabunge 260( ingawa sio wote) kwa sh.Milioni 10 maana yake ni zaidi ya Shilingi Bilioni 2.6(2,600,000,000/=) ambazo zingeweza kutumika kununua madawa.
Wanafunzi walionyimwa Mikopo Vyuoni tena watoto wa Maskini wanajiskiaje wao na wazazi au ndugu zao wanaposikia Serikali inafanya mambo ya aibu kama haya?
Ndugu Zetu kule Kagera bado hawana makazi ya kudumu.Hawana vyakula.
Serikali na Chama Tawala wanatumia Mabilioni kuhonga Wabunge kupitisha Mswada ambao unavunja haki za kikatiba za kuzuia watanzania kupata habari.
Mabilioni yanatumika kurutubisha mbegu za Udikteta wakati watanzania wanakabiliwa na Maisha Magumu huku vijana wakikosa ajira.
Mwenyekiti wa Chama Tawala John Magufuli alikua akijinasibu kuwa Mpambanaji dhidi ya Ufisadi.Katibu Mkuu wake Kinana hawezi kufanya haya bila Magufuli kujua.
Waziri Mkuu hawezi kuhudhuria kikao cha aina hiyo bila Rais Kujua.
Nchini Uganda Rais Museveni alivyopeleka Mswada wa Marekebisho ya Katiba alihonga Wabunge wa chama cha NRM na kutumia Taasisi fulani ambayo ina kampuni Rafiki na Chama Tawala.
Wabunge wakahongwa kilo 50 za Sukari na Dola Elfu 10.
Imekuwa Tabia ya Rais Kagame alipobadili Katiba na Pia alifanya Hivyo Mobutu Sese Seko
Bunge ni Chombo cha Wananchi kuwasemea na kuusimamia Utawala.Utawala unawahonga Wabunge wasifanye kazi ya Wananchi.
Hiki ndicho alichoandika Dr.Roger Tangri na Andrew Mwenda katika kitabu maarufu cha
"The Politics of Elite Corruption in Africa:Uganda in Comparative Perspective"
Alielezea jinsi watawala wanavyotumia Raslimali za Umma kupitisha mambo yao na kujiweka Madarakani bila kuhojiwa na bila misukosuko.
Tangu Magufuli amteue Dr.Tulia Kuwa Mbunge ilikua Maandalizi ya yeye kuminya Demokrasia kwa kuling'oa Bunge Meno.
Huyu ndiye Magufuli ambae kesho atahutubia kujisifu kuwa ni Rais wa wanyonge na Mchukia Ufisadi.
Watanzania Tuungane Kuulaani na Kuupinga Unafiki na Ufisadi huu ndani ya Bunge.
A Luta Continua,Victory Ascerta....
Ben Saanane
Source Ben Saanane Page

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI