Tundu Lissu ahojiwa kwa kumwita Rais Magufuli "Mtakatifu". Aachiwa... - MULO ENTERTAINER

Latest

31 Dec 2016

Tundu Lissu ahojiwa kwa kumwita Rais Magufuli "Mtakatifu". Aachiwa...


Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo 
(CHADEMA) ameachiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam na
pia polisi mkoa wa kipolisi Ilala.



Amehojiwa ni kwanini anamwita Mheshimiwa kuwa ni Mtakatifu. 



Amehoji akiita "lile jina" ambalo limemfanya awe na kesi kadhaa mahakama ya Kisutu ni shida. Je, na hili la Mtakatifu ni shida? 



Amehojiwa aeleze maana ya Mtakatifu akaeleza ni asiye na hatia mbele ya Mungu na wanadamu. 



Amehojiwa pia kuhusu kikosi kazi kinachotesa watuhumiwa wanaokuwa chini 
ya polisi lakini huchukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha mateso na 
kurejeshwa alfajiri Central. 



Amewaambia yeye ameongea na walioteswa na kuna wapo walio tayari kutoa ushahidi kuhusu ukatili wa kikosi kazi hicho. 



RCO wa Ilala amekana na kusema kuwa watuhumiwa huwa hawateswi. 



Lissu pia amehojiwa kuhusu sakata la kupotea Ben Saanane na polisi 
wanavyoweza kumtafuta amewaambia watafute mawasiliano yake ya mwisho 
waseme Saanane yuko wapi. 



Lissu amekuwa polisi akiwa na Wakili Fred Kihwelo tangu saa nne hadi saa kumi na nusu.



Polisi wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu maelezo hayo.