Polisi wanamtafuta kijana anayetuhumiwa kuwa muuaji sugu maarufu Mpemba ambaye pia anakabiliwa na makosa mengine mbalimbali.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro ametangaza dau la Sh5 milioni kwa mtu yeyote atakayempata mtuhumiwa huyo au kutoa taarifa zitakazowawezesha kukamatwa.
“Ni jambazi sugu na anafanya mauaji, hovyo ameanza muda mrefu tangu kipindi cha Kamanda (Suleiman) Kova ametangazwa lakini hadi leo hii hajakamatwa,” amedai.
Licha ya Mpemba, jeshi hilo linamtafuta kijana mwingine wa Mkuranga mkoani Pwani ambaye anatuhumiwa kuchukua wake wa majambazi wenzake ambao wamekamatwa na Polisi na kuwaozesha kwa wahalifu wengine.