News Alert: Rais Magufuli Amteua Meneja Kampeni Wake Kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2015 Kuwa Mbunge..!! - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Jan 2017

News Alert: Rais Magufuli Amteua Meneja Kampeni Wake Kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2015 Kuwa Mbunge..!!

 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhmi ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 16 Januari, 2017 amefanya uteuzi wa Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuii ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja.

Wabunge walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Majula Bulembo na Prof. Palamaganiba John Aidan Mwaluko Kabudi. Wabunge wateule hawa wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi. Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa baadaye.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU
Dar es Salaam
16 Januari, 2017