|
Babu Tale |
Babutale ni meneja maarufu wa kundi la bongofleva la Tip Top connection
lakini pia ni meneja wa mwimbaji Diamond Platnumz ambapo leo Tale
ameguswa na baadhi ya video kadhaa za bongofleva baada ya kuzitazama
akaandika haya.
"Hii ni kwa ndugu zetu madirector wa nyumbani tanzania, tunaomba angalau
muwe mnajishugulisha kuangalia vitu ambavyo havijatumika ili kuepuka
kufananisha video zetu,sababu inapelekea wasanii kukimbia na kwenda
kufanya kazi zao nje ya nchi"
"Mfano kuna video ya dogo janja na roma zote location moja,madee bilnas
na wengine wote wametumia vitoa moshi,chege na ben paul wote wametumia
gari moja,hilikosa ni la msanii au director?
#kelele_za_chura@chegechigunda"