moja ya vitu vigumu zaidi kuacha duniani ni sigara, ni watu wachache
sana wenye juhudi kubwa hufanikiwa kuacha sigara kutokana na kiasi cha
kemikali ya nicotine kilichoko ndani ya sigara ambacho kinamfanya
mtumiaji apate kiu kali ya kutaka kuvuta sigara pale anapojaribu kuacha.
ukiwa unaanza kuvuta sigara huwezi ukajua kua ipo siku utakuja kua
mtumwa wa sigara lakini baada ya miaka kadhaa ndio utagundua kwamba
umekua mtumwa na kuacha huwezi..
watafiti wamejitahidi kutafuta suluhisho la sigara na kugundua baadhi ya
dawa , pamoja na kutumia dawa hizi mtumiaji lazima pia atumie njia
kadhaa za kuacha ambazo sio za dawa kama kuamua moyoni kwamba ameamua
kuacha, kukaa mbali na wavutaji sigara, kuanza mazoezi yeyote ya mwili
ambayo kimsingi husaidia sana kuponya addiction, kula vizuri na
kupumzika, kuepuka kutumia vilevi vyovyote ambavyo vitamrudisha huko na
hata kuonana uso kwa uso na mshauri wa afya.
dawa zifuatazo zimesaidia baadhi ya watu kujikomboa na uvutaji wa sigara
bupropion; hii ni dawa ya mgandamizo wa mawazo ambayo pia
hutumika kutibu watu wanaotaka kuacha sigara, hufanya kazi kwa kuondoa
kiu kali ambayo huipata pale tu anapoacha sigara. mgonjwa hutumia dozi
ya 100mg kutwa mara tatu huku akiendelea kuvuta sigara kisha wiki ya
pili mgonjwa huacha sigara na kuendelea na dawa hizi angalau kwa muda wa
wiki saba.
nicotine; hii ni kemikali inayopatikana ndani ya sigara ambayo
inamfanya mtumiaji wa sigara ashindwe kuacha, hivyo wataalamu
wameichukua kemikali hii na kuiweka kwenye jojo au big g ili mtumiaji
aweze kuila kwa kutafuna jojo hizi kama mbadala wa sigara na baada ya
muda fulani apunguze dozi ya jojo hizi mpaka pale atakapokua ameacha
kabisa na mwili kuzoea kuisha bila nicotine. hutakiwi kutumia zaidi ya
jojo 20 kwa ndani ya saa 24.
clonidine; hii ni dawa inayotumika kutibu presha ya kupanda
lakini pia imethibitika kwamba inasaidia watu kuacha kuvuta sigara,
matumizi yake ni kidonge kimoja kutwa mara mbili....unaweza kuanza
kutumia dawa hii siku ya kuacha au siku tatu kabla ya kuacha na
kuendelea nayo huku ukipunguza dozi kwa siku nne mpaka tano. hutakiwi
kuacha dawa hii ghafla kwani huweza kupandisha presha ghafla.
varenicline; baadhi ya watafiti wanahisi dawa hii inafanya kazi
kuliko dawa nyingi za kuacha sigara, hufanya kazi kwenye ubongo kwenye
sehemu inayoitwa kitaalamu kama nicotine receptors kwa kumfanya mtumiaji
asione raha kuvuta sigara lakini pia huondoa ile kiu mtumiajia
anayoipata pale anapokosa kuvuta sigara. matumizi yake ni wiki mbili
kabla ya kuacha sigara na kidonge kimoja humezwa na maji mengi baada ya
kula. dawa hii huendelea kutumika mpaka wiki 12 na zaidi ili kumsaidia
mtumiaje aache kabisa.
notriptyline; hii ni dawa inayotumika kutibu mgandamizo wa
mawazo, ambayo pia husaidia kutuliza ile kiu mtu anayoipata anapokosa
sigara. huanza kutumiaka siku 10 mpaka 28 kabla ya kuacha kuvuta
sigara..dawa hii hupunguza uwezo wako wa kutumia mashine yeyote ya moto
kwa kipindi hiko.. ni vizuri usitumie mashine yeyote ya moto au
kuendesha gari.
mwisho; dawa hizi zina madhara madogo madogo na makubwa kama
ilivyo kwa dawa zingine, ni vizuri kabla ya kuanza kuzitumia au
kuzinunua uonane na daktari ili ujue kama wewe zinakufaa kwani kuna
baadhi ya dawa hazifai wagonjwa fulani fulani kama wa moyo, kisukari au
madonda ya tumbo. bahati mbaya hata kuzipata hapa nchini kwetu ni
changamoto kidogo lakini kwa watanzania walioko nje wanaweza kuzipata
hata watanzania wa ndani ya nchi wanaweza kuagiza nje kama wanaweza.