Aslay amefunguka sababu iliyomfanya aondoke kwenye nyumba ya kituo cha
Mkubwa na Wanawe,ambapo alipokuwa anaishi Waimbaji wenzake.
Hitmaker huyo wa ‘Angekuona’, amekiambia kipindi cha ‘On The Eight’ cha
TVE kuwa hakuna matatizo yoyote yaliyomsababisha kuondoka katika kituo
hicho bali aliamua kuifuata familia yake ili aweze kuishi nayo kwa
ukaribu, tofauti na watu wengi wanavyofikiria.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa zamani alijisahau zaidi katika muziki,
lakini kwa sasa amepanga kujibrand yeye mwenyewe na kuachia nyimbo zake
mwenyewe ambazo zitamtambulisha zaidi.