Majonzi Kifo cha Mwasisi wa Freemasons Nchini..!!! - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Apr 2017

Majonzi Kifo cha Mwasisi wa Freemasons Nchini..!!!


NI majonzi! Mfanyabiashara maarufu ambaye pia anatajwa kuwa mmoja wa waasisi wa Freemasons nchini Tanzania, Sir Jayantilal Keshavji (Andy) Chande amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.

Ndugu wa karibu na familia alithibitisha juu ya taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo jana kupitia simu akiwa Nairobi nchini Kenya, akisema alifariki jana asubuhi wakati akiendelea na matibabu nchini humo.

Alisema familia yake ilikuwa katika harakati za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka Nairobi kuelekea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.

Chande alizaliwa Mei 7, 1928 mjini Mombasa Kenya, alikulia na kusoma katika eneo la Bukene, wakati huo likiitwa Jimbo la Magharibi nchini Tanganyika kabla ya kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Pune mjini Bombay (sasa Mumbai), India katika miaka ya 1950.

Katika miaka ya 1990 hadi katikati ya mwaka2000, Chande alikuwa kinara wa Freemasons katika ukanda wa Afrika Mashariki na Shelisheli.

Sir Andy Chande amewahi kuandika vitabu mbalimbali, kimojawapo kikijulikana kwa jina la “A Knight in Africa: Jourbey from Bukene”. Ameacha mke na watoto.