Leo ulifanyika mkutano na Waandishi wa habari ukimuhusisha Mkurugenzi
wa vipindi Clouds Media Ruge Mutahaba, RC wa Dar es Salaam Paul Makonda
na Jukwaa la Wahariri kuhusu swala la kufungiwa kwa habari za Mkuu wa
mkoa Paul Makonda.
Baada ya mkutano huo na mengine yaliyojadiliwa na kauli zilizotolewa
ikiwemo ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kusema hawezi kuomba radhi, Ruge
Mutahaba amehojiwa na vyombo vya habari baada tu ya mkutano huo kuisha
na kueleza msimamo wa CLOUDS.
“Baada ya jambo la leo msimamo wa CLOUDS MEDIA GROUP ni uleule tuliokua
nao toka siku ya jumamosi baada ya kupatanishwa na Mh. Rais, siku ile
alivyotupatanisha sisi kama Watanzania hatukua na budi zaidi ya kukubali
na kurudi kwenye uhusiano wa kiuweledi.
“Leo tuliitwa kwenye kikao kwa kutegemea labda kungekua kuna kingine cha ziada lakini…………………………” Amesema Ruge
10 Aug 2017
New