Takriban watu 90 wameuwa kufuatia tetemeko la ardhi la uzito wa 8.1 katika vipimo vya richa nchini Mexico kwa mujibu wa maafisa.
Msemaji wa serikali alisema kuwa watu 71 walikuwa wameuawa katika jimbo lililo kusini magharibi la Oaxaca.
Mamia ya familia zimeripotiwa kushinda katika mitaa, zikihofia hatari za mitetemeko midogo.
Wanajiolojia nchini Mexico wanasema kuwa mitetemeko midogo 721 imerekodiwa tangu tetemeo kubwa la Alhamisi.
Tetemeko hilo lilikuwa la nguvu nyingi zaid kuwai kushuhudiwa nchini humo kwa karne moja.
Siku ya Ijumaa, pwani ya mashariki mwa Mexico ilikumbwa na dhoruba inayojulikana kama Katia.
Watu wawili walifariki kwenye maporoko ya udongo baada ya mvua kubwa.
10 Sept 2017
New