Haya ni baadhi ya mambo 9 aliyoyazungumza mjini Dodoma;
-Tupunguze ukataji miti na uvunaji wa miti uzingatie sheria zilizopo.
-Taasisi za serikali zitunge sheria ndogo za kusimamia shughuli za mazingira.
-Wananchi tuitikie na kutekeleza programu mbalimbali zinazoanzishwa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.
-Hii ni awamu ya kwanza tutaratibu awamu ya pili ya program hii.
-TANROADS iandae utaratibu wa kupanda miti pembezoni mwa barabara.
-Wananchi tuanze kutumia nishati mbadala ili kunusuru mazingira yetu.
-Naagiza kampeni hii isiishie Dodoma Mjini bali ienee katika Wilaya zote za Mkoa huu na hatimaye nchi nzima.
-Upandaji wa miti si kwa ajili ya hifadhi tu bali ni fursa ya kiuchumi pia.
-Kampeni hii ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu Dkt. Magufuli wa kuhamishia Makao Makuu hapa Dodoma.